![]() |
![]() |
![]() |
S.L.P 1219, Musoma - Tanzania Simu +255 28 2620920/2620255 , +255 784 582 786/555: taarifa@juasun.net [ In English ] |
![]() |
![]() |
|
Ndugu mwanachama wa mtandao, ukurasa huu unakusudia kukusaidia kuielewa na kutambua huduma itolewayo na juasun.net na pia kusaidia kutatua baadhi ya matatizo unayoweza kukutana nayo kama vile: -Nitahakikishaje kuwa kompyuta yangu ni salama? -Je Mtandao wangu kwa njia ya mawimbi haupo Nifanyeje?. -Kwa nini inachukua muda mrefu kupataa barua pepe yangu kwa njia ya simu? -Kwa nini nitumie Mozilla? ![]() -Firefox ni nini?-Thunderbird ni nini?Njia tatu za kusaidia kuhakikisha kuwa kompyuta yako ni salama: 1.Tumia ukuta-moto. 2.Pata marekebisho ya Operating System. 3.Tumia programu mpya inayotumika katika kuzuia virusi vya kompyuta. ![]() Mtandao wa Mawimbi ukikosekana: Kunaweza kuwa na sababu kadhaa zinazoweza kusababisha mtandao kwa njia ya mawimbi kukosekana, fanya yafuatayo kuhakikisha kwamba vifaa vyako vya mtandao vinafanya kazi ipasavyo:- - Kagua na kuona kama vifaa vyote vimeunganishwa sehemu zinazostahili. -Jaribu kutembelea tovuti ya juasun.net kwenye mtandao na kuona kama unaweza kuzifikia barua pepe zako. Kama utaweza kuifikia na kusoma barua pepe zako ujue mawasiliano yako ya mawimbi hayana tatizo. Na kama hutaweza kuingia katika akaunti yako ya barua pepe au katika mtandao, tujulishe kwa njia ya simu kwa msaada zaidi. Barua pepe zinachukua muda mrefu kufunguka kwa kupitia njia ya simu: -Hii inaweza kusababishwa na kuwepo kwa barua pepe kubwa katika akaunti yako, Barua pepe hiyo inaweza kuwa imeambatanishwa na faili kubwa nyingine kwa mfano, picha. Kama unaweza kufungua tovuti ya Juasun.net, Futa barua hiyo kama si ya muhimu, vingenevyo tunashauri kutumia Internet cafe kusoma na kuhifadhi hiyo barua katika floppy diski, alafu kuifuta kutoka katika akaunti au tutembelee/piga simu ofisini kwetu Musoma kwa msaada zaidi. Mozilla * Kwa kutandaa, barua pepe, kuhariri HTLM, IRC chat na zaidi. * Imetengenezwa kulinda usalama wa taarifa zako. * Zuia vichomozi na barua-taka. * Fungua kurasa nyingi katika dirisha moja. Firefox Brauza ya kizazi kipya iliyoshinda Tuzo ni ishara ya vitu vijavyo kutoka Mozilla. Ni yenye nguvu na rahisi kutumia. Ni sahihi kwa wale waishio kisasa. Thunderbird -Ni programu ya Barua pepe na habari mpya yenye nguvu ya kudhibiti barua-taka. |