P.O Box 1219, Musoma - Tanzania
Tel +255 28 2620920/2620255 , +255 784 582 786/555: taarifa@juasun.net      [ In English ]
  ->Juasun > Kuhusu sisi

Miradi
Faharasa
Tovuti nyingine
Tuma Maoni


Juasun.Net ni Kampuni itoayo huduma ya mtandao wa mawasiliano ambayo kwa sasa inahudumia maeneo ya vijijini nchini Tanzania. Tunatoa huduma ya aina zote za mawasiliano ya mtandao kwa kupitia njia ya mawimbi na simu kwa gharama nafuu. Na pia huduma nyingine zinazopatikana ni Sauti kupitia mtandao (VOIP), Telemedicine, Maabara ya Kompyuta zitumiazo jau(solar), huduma kupitia nyaya nyembamba (nyuzi nyuzi - Fiber) na pia Uenyeji wa Tovuti ndani ya Tanzania.

Leseni Juasun.Net imesajiliwa na kupata leseni chini ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

MALENGO:
Lengo la Juasun.net ni kusaidia katika kuendeleza teknolojia ya mawasiliano na kusambaza habari vijijini nchini Tanzania, kwa kiwango cha ubora wa juu pamoja na kuwaelimisha vijana Waafrika waishio vijijini kuhusu teknolojia hii ya Mawasiliano ya Mtandao.

MAHALI TULIPO:
Makao Makuu ya Juasun.net yako Musoma, Mara, moja ya mikoa ya Kaskazini mwa Tanzania inayopakana na Ziwa Nyanza (Victoria) na Serengeti.Pia Matawi yake yako katika Wilaya ya Bunda - Mara na Pangani Mjini - Tanga.


WASHIRIKA WETU
Washirika wetu ni Kampuni ya simu Tanzania (TTCL), Kamishina ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Vyuo vikuu vya Dar es Salaam (UDSM), IFM, Mzumbe, Ruaha, Dodoma, Arusha(Taasisi ya Fedha), Ubiquit Network Inc, Aleutia Ltd, Mamlaka ya Serikali za Mitaa Tanzania, Tanesco na Taasisi ya Teknolojia Royal Stockholm, Sweden.



Copyright © 2010 Juasun.Net, All Rights Reserved.