Juasun.net
ni Kampuni itoayo huduma ya mtandao wa mawasiliano ambayo kwa sasa
inahudumia maeneo ya vijijini nchini Tanzania. Tunatoa huduma ya
aina zote za mawasiliano ya mtandao kwa kupitia njia ya simu na
pia kwa njia ya mawimbi kwa wanachama wetu kwa gharama nafuu.
Juasun.net imesajiliwa na kupata leseni chini ya Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA).
MALENGO
Lengo la Juasun.net ni kusaidia katika kuendeleza teknolojia ya
mawasiliano na kusambaza habari vijijini nchini Tanzania, kwa kiwango
cha ubora wa juu pamoja na kuwaelimisha vijana Waafrika waishio
vijijini kuhusu teknolojia hii ya Mawasiliano ya Mtandao.
MAHALI
TULIPO
Makao Makuu ya Juasun.net yako Musoma, Mara, moja ya mikoa ya Kaskazini
mwa Tanzania inayopakana na Ziwa Nyanza (Victoria) na Mbuga za Serengeti.
|